19 Desemba 2016 - 19:22
Majeshi ya Syria yaendelea kuokoa watu Aleppo mashariki

Operesheni ya kuwaondoa maelfu ya watu kutoka katika eneo lililokuwa linashikiliwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani la Aleppo inaendelea tena leo,

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Operesheni ya kuwaondoa maelfu ya watu kutoka katika eneo lililokuwa linashikiliwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani la Aleppo inaendelea tena leo, baada ya kusitishwa kwa siku kadhaa kutokana na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani, kufanya mashambulizi dhidi ya mabasi ya misaada kwa wananchi zaidi ya 20. pamoja na kuondolewa watu katika vijiji viwili vilivyozingirwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani katika jimbo la Idlib. Msafara wa mabasi kutoka mashariki mwa Aleppo umewasili maeneo yanayoshikiliwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani upande wa magharibi wa mji huo, kwa mujibu wa afisa wa Umoja wa mataifa na shirika linaloangalia haki za binadamu nchini Syria. Wakati huo huo , mabasi 10 yameondoka katika vijiji vya Washia vya Foua na Kefraya, kaskazini mwa Idlib, kwenda katika maeneo yanayoshikiliwa na serikali mjini Aleppo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema jumla ya raia 12,000 wameondolewa kutoka mikononi mwa magaidi wanaoungwa mkono na Marekani Aleppo, ikiwa ni pamoja na wengine 4,500 tangu usiku wa jana. Wakati hayo yanaendelea Baraza la Usalama lapitisha mswada wa kuweka waangalizi Syria

Kwa kuungwa mkono na Urusi, baraza la Usalama la Umoja wa mataifa leo limepiga kura kuweka haraka waangalizi wa Umoja wa mataifa kuangalia uondoaji wa watu na kuripoti hatima ya raia ambao wamebakia katika eneo lililozingirwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani katika mji wa Aleppo, nchini Syria. Baraza hilo kwa kauli moja limeidhinisha azimio lililowasilishwa na Ufaransa ambalo ni mara ya kwanza kuonekana umoja katika miezi kadhaa miongoni mwa mataifa yenye nguvu katika mzozo wa Syria.

Hatua hiyo inaupa jukumu Umoja wa Mataifa kufanya uangalizi wa kutosha bila upendeleo na uchunguzi wa moja kwa moja wa watu wanaoondolewa kutoka mashariki mwa Aleppo na wilaya nyingine za mji huo. Azimio hilo linataka kwamba katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon achukue hatua muhimu kuruhusu waangalizi kuhakikisha kwamba raia wanapata mahitaji muhimu na kushauriana na pande zinazohusika kuhusiana na wapi watu hao watawekwa.

Serikali ya Urusi iliunga mkono mswada huo ulioletwa na Ufaransa baada ya kukosoa na kubadilisha vipengele vinavyotetea magaidi katika mswaaada huo.

Mwisho wa habari/ 291